Shauri ni
kijana wa kwanza kuzaliwa katika familia ya watoto watatu,kazaliwa kutoka
katika familia ya kimaskini yeye na wadogo zake Fadhil na Justine, na ni
wakazi wa mkoa wa Mbeya. Baba yao alifariki na mama yake alikuwa ni mkulima
mdogo asiye na uwezo wa kumudu baadhi ya mahitaji ya familia.Kijana Shauri alikuwa na bidii sana katika
kazi mbali mbali za nyumbani na shule japo majukumu ya nyumbani yalimzidia na
wakati mwingine alilazimika kwenda shamba kumsaidia mama yake shuguli za shamba
badala ya kwenda shule.Walimu wake hawakujua tatizo lake hivyo alikabiliwa na
adhabu kila alipokosekana shule.Kijana
Shauri alijitahidi sana kuwasaidia wadogo zake katika shughuli za nyumbani
kama vile kufua,kuwaogesha na kuwapikia.
Baada ya miaka kadhaa kijana
alihitimu shule ya msingi na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika
shule ya kata pale kijijini kwao, kijana alichelewa kuanza kidato cha kwanza
kutokana na changamoto ya kiuchumi lakini hata hivyo alijiunga na wenzake na
kuanza masomo rasmi mwezi wa pili, kijana alisoma kwa bidii na pamoja na
misukosuko mingi alijikuta akipendwa sana na walimu sababu ya kujituma kwake
ndani na nje ya darasa.alipofika kidato cha tatu mdogo wake wa pili aitwaye
fadhil nae alijiunga na kidato cha kwanza hivyo kufanya mambo kuwa magumu sana
kwa mamayao kwani hakuweza kumudu gharama za kuwasomesha watoto wawili hivyo
ikamlazimu kijana Shauri kuanza kufanya vibarua mbalimbali mtaani kwaajili ya
kutafta pesa za karo yake na ya madogo wake hata hivyo kijana alifanikiwa
kuingia kidato cha nne. Akiwa kidato cha nne kijana alisoma kwa bidii sana na
hatimaye alihitimu.
Baada ya muda matokeo
yalitoka na yakawa mazuri kijana alifaulu kujiunga na kidato cha tano katika
shule moja mkoani Kigoma,kijana alihangaika huku na kule kutafuta msaada
hatimaye alipata ufadhili wa mtu binafsi aliyejitolea kumsomesha.Kijana
alijiunga na kidato cha tano na baada ya muhula mmoja kwa bahati mbaya alipata
taarifa za kifo cha mfadhili wake.Shauri alilia sana huku akijiuliza ni kwa
namna gani ataweza kusoma tena kwani mama yake hakuwa na uwezo kabisa,na tangu
Shauri aende shule hakuwahi kurudi nyumbani kutokana na changamoto ya
nauli.kijana alimshirikisha Mwalimu wake juu ya tatizo hill na mungu si athumani
Mwalimu aka ahidi kumsaidia kulipa karo.Pamoja na misukosuko yote kijana
alisoma kwa bidii sana na kufaulu vema kwenye masomo yake na hatimaye alihitimu
kidato cha sita.Kijana alimshukuru sana Mwalimu wake kisha akasaidiwa nauli na
kurudi nyumbani ambako familia yake walimpokea kwa Furaha sana ndugu yao.Kwa
kuwa ulikuwa msimu wa kilimo kijana alimsaidia sana mama yake katika shughuli
za shamba kwa kipindi chote cha kusubili majibu, na hatimaye majibu yalitoka
yakiwa mazuri kijana kafaulu kuingia chuo kikuu.Alifurahi sana ila ghafla
akaingiwa na huzuni baada ya kukumbuka adha za karo alipokuwa shule.Kwa bahati
nzuri kijana alipata mkopo hivyo akajiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam akisomea shahada ya
sheria.Akiwa anakaa hostel alipata kufahamiana na marafiki kadhaa na kubwa
zaidi alianza kuona watoto wakike wazuri ambao kijijini kwao hakufanikiwa
kuwaona,Hakika alitaman naye sikumoja awe na mpenzi kama wenzie
walivofanya.Katika kikundi cha kujisomea Kwa bahati nzuri nae alifahamiana na mdada mmoja aitwaye victoria mtoto aliyetoka katika familia
ya kitajiri.walipata kuwa marafiki kwa muda kisha binti alinza kuingiwa na hisia
za mapenzi kwa kijana Shauri ambaye
hakuwa na mvuto kwa wadada wengi kwani hakuwa mtanashati kama wana chuo
wengine,kijana alivalia mavazi makuukuu kutokana na kutokuwa na uwezo wa
kununua mavazi mapya.
Victoria alishindwa kuzuia hisia zake
kwa bwana Shauri huruma ilimuingia baada ya kusimulia siku moja historia ya
maisha yake akajikuta akimsaidia Shauri pesa za matumizi pamoja na kumnunulia
mavazi mapya hivyo kubadili muonekano wa kijana lakini bado hawakuwa wapenzi
kwani hakuna aliye weza kumwambia mwenzake.Baada ya kuingia mwaka wa pili
kijana alikosa mkopo kutokana na mabadiliko ya kielimu na hivyo maisha kumuwia
magumu,kijana hakusita kumwambia rafiki yake Victoria nae akamtoa wasiwasi na
kumsaidia pesa nyingi ambazo alilipa ada na akabakiwa na pesa za kutosha zilizo
muweka mjini.
Baada ya muhula mwingine wa masomo
Victoria alimwambia mama yake kuwa kampata rafiki ambaye anategemea aje kuwa
mume wake baadaye lakini hakuwahi kumwambia
Shauri kuhusu hisia zake.Kijana SHAURI alijua ni urafiki tu na aliogopa
kumwambia vick kuwa anampenda kwani aliogopa anaweza kupoteza msaada ikiwa vick hatakuwa tayali kwa uhusiano
huo.Alijikuta akianza kumpenda binti nwingie aitwaye Janeth na kwakuwa
muonekano wake wa sasa ulikuwa na mvuto kwa wadada wengi,haikumsumbua kumwambia
janeth naye alikubali kuwa wawe wapenzi.
Mtoto wa kitajiri Victoria
aliendeleza urafiki na kijana Shauri na kuendeleza msaada wake kwa kijana,huku
kijana Shauri akianza kutumia murua kabisa pesa anazopewa na Victoria kutanua
au kula na mtoto Janeth.Shauri alifanya siri uhusiano wake huo lakini kwa mtoto
Janeth ilikuwa tofauti alijiachia sana na kuwatambulisha marafiki zake,ikumbukwe
wakati huu kijana SHAURI alikwishakuwa mjanja akimiliki simu janja na kompyuta
kwa msaada wa Victoria, hivyo walikuwa wakipiga picha akiwa na mtoto Janeth na
kuziacha kwenye simu janja yake.
Mtoto Victoria naye hisia
zilimzidia akahisi sasa ni wakati mubashara kabisa wa kumwambia kijana Shauri kuwa wawe wapenzi rasmi,binti alijiandaa
kisha akamwomba Shauri wakutane
hoteli moja hapa jijini siku ya jumamosi ambayo sio ya masomo,binti alijiandaa mapema siku
hiyo kwa kuvaa nyuzi mpya watoto wa mjini wanaita viwalo vipya,marashi ya
harufu nzuri na ya bei mbaya sana,nywele zimeandaliwa vema kabisa pamoja na
viatu vyake virefu aliwasili hotelini na kumsubili kijana,huku upande wake kijana Shauri yeye kwa upande wake hakuwahi
kuingia hoteli kubwa namna ile naye alijiandaa vema siku hiyo akavalia murua
mavazi yake mapya aliyonunuliwa na rafiki yake Victoria na kuelekea hotelini........Je! unajua nini kitatokea baada ya shauri kuwasili?
Je! Msichana mrembo Vicky atafunguka hisia zake? Na shauri Je! Atakubali amuache Janeth
mpenzi wake? Usipitwe na episode ya pili.
ITAENDELEA Episode O2………
Written: by Jelly Mbwilo
Edited :by Masomo Yetutz blogger.
Approved :by Samuel Ilomo
visit: www.masomoyetu.co.tz
visit: www.masomoyetu.co.tz
Comments
Post a Comment