JOGOO SHAMBA EPISODE 2
Ilipo ishia
"mrembo Vick alimualika kijana Shauri katika hoteli moja ya kifahari,na
akawasili akiwa kapendeza kwa kutupia viwalo vya bei mbaya na kupendeza murua
kabisa,huku kijana Shauri nae akitokelezea vilivyo"
"Inaendelea"
Mrembo Vick alifika mapema hotelini hapo na kumsubiri mpemzi wake huku
akiwa anashushia glass ya wine taratiibu,kijana nae aliwasili hotelini na
kuelekea moja kwa moja pale alipokuwa ameketi mpenzi wake.Wakakumbatiana kwa
bashasha kabisa huku kila mmoja akiwa amejawa na huba juu ya mwenzie kisha
wakaketi,Vick akammiminia glass ya wine bwana Shauri kisha wakaanza mazungumzo
yao huku wakitazamana usoni.
Mrembo Vick alimweleza mzee baba Shauri juu ya malengo aliyo nayo juu
yake kwamba anatamani waje kufunga ndoa na kuishi pamoja na Shauri pia
alimuunga mkono juu ya suala hilo.Wakati mazungumzo ya wapendanao yakiendelea
ghafla alikatiza mrembo Janeth akiwa na mwanaume mwingine,ikumbukwe Janeth pia
ni mpenzi wa kando wa mzee baba Shauri,basi macho yakamtoka bwana Shauri kama
vile kabanwa na mlango ila kwasababu yupo na bibie Vick ikabidi ajifanye yupo
sawa.Mrembo Vick hakuwa mchovu alishuhudia kuduwaa kule kwa mpenzi wake kisha
akamuuliza kama kuna tatizo bwana Shauri akakanusha kuwa yupo sawa kabisa basi
stori zikaendelea.
Baada ya muda yule mwanaume aliyekuwa na mrembo Janeth alitoka na kwenda zake
kisha akabaki Janeth pekeyake na alikuwa akinywa pombe Kali sana na kulewa
sana,kwa bahati mbaya Janeth aliinuka na kuanza kutoka nje lakini alipita
karibu na walipokuwa wamekaa Shauri na Vick na ghafla akawaona wakiwa
wamekaribiana sana,huku bwana Shauri akijiinamia ili asionekane lakini wapi
alionekana na moja kwa moja Janeth aliwafata na kuanza kumuhoji bwana Shauri
kuwa huyu ni nani huku akionekana kuwa anazidiwa na pombe. Bwanashauri
alijaribu kujikausha lakini mrembo aliendelea kuuliza kwa nguvu na kusema maovu
yake mengi mbele ya Vick,Shauri alishindwa kujibu chochote kwa aibu na hatimaye
mrembo Vick aliinuka na kukimbia nje huku akiwa analia kwa uchungu sana
.......je nini kitaendelea je Shauri atamfanya mini Janeth je Vick atachukua
uamuzigani usikose episode ya 3..
Comments
Post a Comment