TAJILIKA NA UFUGAJI WA KUKU KWA NJIA BORA
UTANGULIZI
Ufugaji wa kuku umekuwa ukifanywa na watu wengi katika
jamii,kwa kulenga Zaidi katika kuinua uchumi wao,kutumia kwa kitoweo na matumizi ya mbolea mashambani na
bustanini.Watu hawa hufuga kwa njia ambazo si za kisasa kutokana na kutokua na
Elimu juu ya uzalishaji au ufugaji wa kuku.
Namna
Ya Ufugaji Wa Kuku Kwa Njia Bora
1.Maandalizi
ya banda
Banda linalo stahili katika ufugaji bora ni
lile lenye sifa zifuatazo:-
a. .Linaruhusu
mwanga na hewa kupita{ventilation}
b. Ni
kavu muda wowote na haliruhusu unyevu kupita au kupenya kama mvua
c. Lisiwe
lina ruhusu wadudu kama nyoka,nge kupita au kupenya.
d. Liwerahisi
kufanya usafi kwa wakati.
e. Lisikaribiane
na banda jingine jirani la kuku ili kuzuia maambukizi ya magonjwa.
2.Matayalisho Kwa Kuwaweka Kuku Wako
Katika Banda
Matayarisho
ya kuwaweka kuku katika banda lako inategemeana na aina ya kuku ambao
umewaandaa au umeanzia kuwafuga.
i.VIFARANGA
Katika maandalizi
ya mahali pakuwaweka vifaranga wenye siku moja au Zaidi panahitaji umakini ili
kukwepa au kuondokana na vifo vya vifaranga
Maandalizi ya Brooder
kwaajii ya kulea vifaranga.
a. Pima
eneo la chumba ambacho umekiaandaa katika banda lenye sifa zote na ujue ukubwa wa eneo katika upana na urefu kwa
kutumia tepu.
b. Na
ukijua urefu na upana wa chumba chako chukua urefu zidisha kwa upana uliopata
mfano {upana10m*urefu 5=50}.
c. Ukishapata
jumla ya ukubwa wa chumba chako jiulize unataka kufuga vifaranga vingapi kwani
kitaalamu vifaranga 10 vinafugwa kwenye mita moja kwa mfano hapo juu mimi
nimepata jumla 50mita za chumba changu kwa hivo vifaranga visivyo zidi 50
nahitaji kufuga katika eneo langu.
Vitu
Vinavyo Hitajika Katika Maanadalizi Ya Brooder
i.
Malanda ya mbao
ii.
.Mifuko ya nailoni au salufeti.
iii.
.Majarida
iv.
Singi board.
Maandalizi ya brooder.
i.
Chukua kiasi cha Maranda mwaga katika eneo
lako ulilo pima na kujua idadi ya vifaranga utakavyo weka Mwaga kiasi cha
sentimita 3 hadi 4kutoka chini.
ii.
Chukua mifuko yako ya nailoni tandika pale
ulipo mwaga Maranda.
iii.
Chukua majarida yako ya tandike juu ya
mifuko ya nailoni.
.
KUPATA NAKALA ZAIDI YA KITABU AU PDF WASILIANA NASI SIMU NAMBA : 0762039071 AU 0625511488 PIA WAWEZA ULIZA SWALI LOLOTE KWA KU COMENT HAPA.
Comments
Post a Comment